Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la AhlulBayt (a.s) - ABNA- leo nchini Lebanon imeadhimishwa kama “Siku ya Shahidi”, ambapo wananchi wa Beirut pamoja na wapiganaji wa Hizbullah wameandaa programu maalum ya kuwaenzi mashahidi wa muqawama (upinzani wa kidini na kitaifa).
Sheikh Naeem Qassem, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah, katika hotuba yake maalum kwa mnasaba wa Siku ya Shahidi, amesisitiza juu ya hadhi tukufu ya mashahidi na umuhimu wa kuendeleza njia ya mapambano ya muqawama.
Akinukuu maneno ya Sayyid Hassan Nasrallah, alisema: “Tunapopata shahada, tunapata ushindi.”
Shahidi hakubali kuishi katika udhalili; kwa imani, ujasiri na kujitolea, anaendeleza njia ya uhuru na kujitegemea.
Akiendelea, Sheikh Qassem aliongeza: “Siku ya Shahidi si tu kwa ajili ya kuwakumbuka mashahidi, bali pia ni heshima kwa familia zao na wote wanaounga mkono njia ya mapambano.”
Alitaja mifano ya mashahidi mashuhuri kama Sheikh Raghib Harb, Sayyid Abbas al-Musawi, na Haj Imad Mughniyeh kuwa ni vielelezo vya kujitolea na uaminifu kwa njia ya muqawama.
Aidha, alisisitiza juu ya kuunga mkono walinzi wa mipaka ya Lebanon, akieleza kuwa: “Lengo la Marekani na Israel kwa sasa si tu kulinda usalama wa Israel, bali ni kuingilia siasa, uchumi, na muundo wa jeshi la Lebanon, ili kudhoofisha uwezo wa nchi hii.”
Your Comment